Cuba yatafuta mwafaka na Marekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cuba huenda ikarejesha mahusiano na jumuia ya umoja wa ulaya

Serikali ya Cuba imesema ina matumaini kuwa Marekani itafuata mfano wa Umoja wa Ulaya,ambapo mwanzoni mwa juma hili ulikubali kuanza mazungumzo yanayolenga kurejesha mahusiano na nchi hiyo.

Umoja wa ulaya unatarajia kuanza mazungumzo na Cuba mwezi ujao.

Waziri wa mambo ya nje wa Cuba, Bruno Rodriguez,amesema Rais wa Marekani Barack Obama anapaswa kuendelea na ari hiyo.

Marekani iliiwekea Cuba vikwazo vya kiuchumi kutokana na sera zake za kiuchumi na rekodi ya haki za binaadam mwaka 1962.

Kauli hii ya Rodriguez aliitoa mjini Havana alipofanya mazungumzo na kamishna wa maswala ya elimu wa Umoja wa ulaya, Androulla Vassiliou.