Misaada zaidi yahitajika Syria

Image caption Mamilioni ya wakazi wa nchini Syria wameyahama makazi yao

Mkuu wa maswala ya kibinaadam ndani ya umoja wa Mataifa,Valerie Amos ametoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhakikisha kuwa misaada zaidi inafikishwa Syria.

Akitoa wito wa azimio hilo,amesema haikubaliki kuona serikali ya Damascus na waasi wakiendelea na vitendo vya kukiuka sheria za kuwafikishia waathiriwa misaada.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limekua likipata mataizo ya kupeleka misaada Syria ambako mamilioni ya raia wa nchi hiyo wameyakimbia makazi yao.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini humo majuma ya hivi karibuni, pande mbili zikiwania maeneo ili kuongeza nguvu zaidi katika mazungumzo yanayoendelea mjini Geneva, nchini Switzerland.

Upande wa serikali ya Rais wa Syria, Bashar al-Assad na makundi ya upinzani bado hawajaafikiana katika ajenda zao, hata hivyo mpatanishi wa mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi ana matumaini kuwa suluhu itapatikana.