Njama ya Nazi kuua watu kwa Malaria

Haki miliki ya picha Robert Seder
Image caption Vimelea vya Malaria

Mwanabayologia mmoja nchini Ujerumani amesema kuwa amepata ushahidi kuwa utawala wa Nazi uliokuwa unaongozwa na Adolf Hitler, ulikuwa unalenga kutumia Mbu kama silaha wakati wa vita vya pili vya dunia.

Klaus Reinhardt kutoka chuo kikuu cha ├╝bingen, alichunguza kumbukumbu za kitengo cha utafiti kilichokuwa katika kambi moja ya mauaji ya Dacahu mwaka 1944.

Anasema aligundua kuwa amri hiyo ilitolewa na mkuu wa kitengo cha jeshi, Heinrich Himmler.

Reinhardt anasema kuwa wanasayansi walikuwa wanajaribu kupata Mbu ambaye angeambukizwa vimelea vya Malaria na kuwaeneza katika maeneo ya maadui kwa wingi ili waweze kuwaambukiza watu wengi iwezavyo

Inajulikana kuwa wafungwa waliokuwa wanusbiri kuuawa katika kambi hiyo waliambukizwa ugonjwa wa Malaria.

Duru zinasema kuwa mipango hiyo haikufanikiwa kwa sababu wajerumani walikuwa wanashambuliwa vikali wakati huo wa vita.