Wachimba migodi wakwama mgodini A.Kusini

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mgodi

Waokozi nchini Afrika Kusini wanafanya kila juhudi kuwaokoa wachimba migodi wengi wanaohofiwa kukwama ndani ya mgodi wa dhahabu.

Waokozi hao wanasema kuwa wameweza kuwasiliana na wachimba migodi hao wanaokisiwa kuwa 30.

Wamekwama kutokana na mawe makubwa yaliyo ndani ya mgodi huo karibu na mgodi mwingine mpya wa dhahabu viungani mwa mji wa Johannesburg.

Wameelezea kuwa wachimba migodi wengine miambili wako ndani ya machimbo ingawa haijulikani ikiwa wamejeruhiwa.