Mlipuko kwenye basi la watalii Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rasi ya Sinai huwa imelindwa vikali na majeshi ya Misri

Taarifa kutoka nchini Misri zinasema kuwa mlipuko kwenye basi katika rasi ya Sinai umewaua watu 3.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la mpaka wa Misri na Israel.

Polisi nchini Israel wanasema kuwa walisikia mlipuko kutoka upande wa Misri katika eneo la Taba ambalo hutumiwa kama kivukio mpakani.

Mlipuko huo ulitokea baada ya basi hiyo kuingia upande wa Misri kutoka Israel .

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda kuna majeruhi wengi.