Mawakili wa Morsi waondoka mahakamani

Image caption Mohammed Morsi akiwa mahakamani

Mahakama moja mjini Cairo Misri imeahirisha kesi ya aliyekuwa Rais Mohammed Morsi, baada ya mawakili wake kuondoka mahakamani kwa hasira.

Mawakili hao wanalalamikia kile wanachosema ni kuendelea kuzuiliwa kwa Morsi pamoja na waliokuwa wanachama wa vuguvugu wa Muslim Brotherhood ndani ya chumba cha Glasi ambacho hakipitishi sauti.

Duru zinasema kuwa mahakama itateua mawakili wengine kumtetea Morsi.

Kesi dhidi ya Morsi itasikilizwa tena Jumapili Ijayo

Rais huyo wa zamani alipinduliwa na jeshi mwezi Julai baada ya kutuhumiwa kwa kupanga njama na nchi za Magharibi , utawala wa Pallestina Hamas, kundi la Hezbollah nchini Lebanon na serikali ya Iran kupanga mashambulizi nchini Iran.

Hii ni moja ya kesi nne zinazomkabili Morsi pamoja na maafisa wakuu wa Muslim Brotherhood.

Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.