Venezuela yawatimua maafisa wa Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Venezuela wakiwa katka maandamano

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amewafukuza maafisa wa ubalozi wa Marekani nchini Venezuela, akiwatuhumu kuonana na wanafunzi waliojihusisha na maandamano dhidi ya serikali.

Kumekuwepo na mvutano wa kisiasa na mikutano,huku watu watatu wakipoteza maisha katika maandamano juma lililopita.

Hati imetolewa ikitaka kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani, Leopoldo Lopez,ambaye ametangaza kuongoza maandamano yatakayofanyika siku ya jumanne mjini Caracas.

Marekani imeeleza kusikitishwa na hatua ya kukamatwa kwa viongozi wa upinzani.

Jumamosi juma lililopita, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alitoa tamko akionesha kusikitishwa kwake na mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Venezuela.