Zoezi la uokoaji lasitishwa A.kusini

Haki miliki ya picha c
Image caption waokoaji wakiwa katika jitihada za kuwaokoa wachimbaji walionasa

Operesheni ya kuokoa wachimba madini walionasa katika mgodi wa dhahabu karibu na mji wa Johanesburg nchini Afrika kusini imesitishwa.

Mpaka hivi sasa wachimbaji 11 wameokolewa kutoka shimoni.

Wachimbaji wengine walionaswa wanaoelezwa kuwa haramu wamegoma kutoka shimoni baada ya kubaini kuwa watatashikiliwa na Polisi.haijafahamika wangapi bado wamenasa ardhini, lakini kuna taarifa kuwa kuna takriban wachimbaji 200 shimoni

Ofisa wa huduma za dharura Werner Vermaak amesema Operesheni hiyo haitaanza tena mpaka pale wachimbaji watakapoomba.

Maofisa wameiambia BBC kuwa eneo la mgodi litakuwa chini ya kampuni ya ulinzi, ambapo watasaidia kutoa taarifa ikiwa wachimbaji hao watabadili mawazo, pia watazuia shughuli za uokoaji ambazo zitafanyika bila kuidhinishwa.

Vermaak amesema kuwa wachimbaji hao hawatanyimwa msaada ikiwa watauhitaji, na wataokolewa pale watakapotaka wenyewe kutoka nje lakini watakamatwa mara baada ya kutoka nje ya shimo walimonasa.