Pellegrini: City ni bora kuliko Man U

Haki miliki ya picha PA
Image caption Manuel Pellegrini

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa timu yake ni bora kushinda bingwa mtetezi wa ligii ya Uingereza Manchester United.

Na kwa sababu hiyo anashikilia kuwa timu yake iko tayari kukabiliana na Barcelona hivi leo kwenye mechi za timu kumi na sita katika ligii ya klabu bingwa barani ulaya.

Raiya huyo ya Chile ameongeza kuwa anaridhia rekodi ya Manchester United ila matokeo ya timu hiyo ya David Moyes yanaonesha kuwa kuwa ni vigumu kuifikia Manchester City kwa vyovyote vile.

Manchester City ni ya tatu kwenye jedwali la msimamo wa ligii kuu ya England, alama tatu nyuma ya viongozi Chelsea, wakati Manchester United ikishikilia nafasi ya saba nyuma ya Liverpoool na Tottenham ambayo iko katika nafasi ya tano ilhali Everton ni ya sita.

Wakati huo huo Manchester United watakuwa uwanjani dhidi ya Olympiakos ya Ugiriki katika ligii ya klabu bingwa barani ulaya.