Mawaziri wa kigeni wawasili Kiev

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uharibifu mjini Kiev

Mabalozi wa Ufaransa, Ujerumani na Poland wamewasili muda mchache uliyopita katika mji mkuu wa Ukraine Kieve ilikufanya mazungumzo ya dharura kuhusiana na mapigano yaliyozuka upya.

Mkutano wao unawadia saa chache kabla ya kufanyika kwa mkutano maalum wa jumuia ya Ulaya kuamua iwapo itaiwekea vikwazo vya kiuchumi Ukraine.

Mazungumzo hayo yanatukia masaa machache baada ya Rais Viktor Yanukovych na viongozi wa upinzani kukubaliana kukomesha uhasama, jijini Kieve na kwingineko Ukraine kwa siku mbili zilizopita.

Awali Rais wa Ukraine, Viktor Yanukovych, na viongozi wa upinzani walitangaza kuwa wameafikiana kusitisha ghasia kali za hivi maajuzi kati ya polisi na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu Kiev na kwengineko.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makabiliano mjini Kiev

Kufuatia mazungumzo na viongozi watatu wakuu wa upinzani, rais Yanukovych alitoa taarifa rasmi iliyosema kwamba walikubaliana kujadiliana yalionuiwa kusitisha umwagikaji damu. Viongozi wawili wa upinzani Vitali Klitschko na Arseniy Yatsenyuk, wamesema rais huyo alitoa hakikisho kwamba kambi za waandamanji katikati mwa mji wa Kiev hazitovamiwa.

Vitaliy Klitschko, ameiambia BBC amefurahishwa na hatua iliyopigwa mpaka sasa.

Moto unaendelea kuwaka katika bustani ya Independence Square huku waandamanji na polisi ya kupambana na fujo wakiwa katika mkwamo.Naibu waziri mkuu wa Ukraine, Konsti-antyn Gry-shchenko ameiambia BBC kwamba upinzani unahitaji kudhibiti alichokitaja kuwa kundi la wafuasi wadogo ambalo anasema ndilo lililosababisha ghasia hizo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ghasia nchini Ukraine

"Tatizo tunalokabiliana nalo sio upinzani wa kiasa, sana sana linatokana na nguvu za watu wenye misimamo mikali ambao hawasikii upinzani. Wanabuni tatizo kubwa kwa kutumia vurugu na kasoro yao ya kutosikizana. Tunahitaji kupata suluhu ambapo wale wanaowajibika kisiasa watahakikisha kwamba kwamba watu hawa wachache wanaosababisha vurugu wanaulizwa maswali na kuthibitiwa."

Watu wapatao 26 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa tangu kuzuka ghasia hizo siku ya Jumanne.