Iran na mataifa ya Magharibi zapatana

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri wa kigeni wa Iran Javad Zarif na Mjumbe wa EU Catherine Ashton

Maafisa nchini Iran wanasema mazungumzo kuhusu mpango wa Iran wa nuclear yamemalizika kwa makubaliano kuhusu utaratibu utakaofuatwa katika mazungumzo yatakayofuata.

Kulikua na tabasamu wakati mkuu wa sera katika Muungano wa Ulaya Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif waliposimama kutoa taarifa hiyo.

Walisema wametambua mambo yote yanayostahili kujadiliwa katika kipindi cha miezi michache ijayo.

Hata hivyo wanakiri kuwa mwafaka wa mapatano hautakua rahisi.

Mataifa ya magharibi yanataka kuhakikisha kuwa Iran haitaweza kutengeneza mabomu ya Kitonaradi na yanataka pia nchi hiyo kusitisha mradi wake wa nuclear.

Kwa upande wake Iran inasisitiza kuwa mradi huo wa nyuklia ni salama na unalenga kutosheleza utashi wa umeme nchini humo.

Tangazo hilo limewadia baada ya siku tatu ya mazungumzo kati ya mataifa matano yenye nguvu za kinyuklia yaani , P5+1 -ambayo inajumuisha Marekani ,Uingereza Ufansa Uchina Urusi na Ujerumani.

Katika maafikiano ya awali mataifa hayo yaliiruhusu Iran kuuza mafuta ya kima cha dola bilioni nne kupunguza makali ya njaa .

kwa upande wake Iran ilikubali kusitisha utaratibu wa kupiga msasa madini ya uranium kufikia ubora ambao unaweza kutumika kutengeneza bomu la kinyuklia .

Hadi kufikia sasa wakaguzi wa kimataifa wa silaha za kinyuklia hawajaruhusiwa kukagua mitambo ya kinyukilia iliyoko Fordo na ile iliyoko katika kambi ya kijeshi ya Parchin .