EU yashindwa na hali Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wajumbe wa Ulaya wanajaribu kutafuta suluhu kwa mgogoro wa kisiasa Ukraine

Ujumbe wa Mawaziri wa Kigeni wa mataifa ya Umoja wa Ulaya umeondoka mjini Kiev kwa Dharura kutokana na hatari kwa usalama wao.

Ujumbe huo umeondoka bila ya kukutana na maafisa wakuu wa serikali ya Ukraine .

Takriban watu watano zaidi wameripotiwa kufariki katika mapigano yaliyozuka upya leo asubuhi .