Kenya yakana kuwahangaisha wasomali

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wakimbizi wa Somalia wakitoroka vita Somalia

Serikali ya Kenya imekanusha madai kuwa inawahangaisha wakimbizi kutoka nchi jirani ya Somalia na kuwasasabisha warudi nyumbani kwao.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International lilidai kuwa wakimbizi kutoka Somalia wanalazimika kurudi nyumbani kutokana na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Kenya Mwenda Njoka, ameambia BBC kuwa makubalino ya wakimbizi kurejeshwa nyumbani , sio kwa kuwalazimisha bali kwa o kutaka wenyewe.

Miongoni mwa changamoto zilizotajwa ni kuchelewesha usajili wa wakimbizi.

Lakini kwa hilo Bwana Njoka alisema kuwa Kenya inakabiliwa na changamoto ya wakimbizi wengi kuingia nchini humo ikiwemo wakimbizi kutoka Sudan Kusdini ambako vita kati ya waasi na serikali imewalazimisha maelfu kutoroka makwao.

Serikali ya Kenya imesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu 60 wa Somalia wamerudi nyumbani kwa hiari na sio kwa kushurutishwa tangu mkataba wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Somalia kwa hiari utiwe saini Oktoba mwaka uliopita.

Amnesty International ilitoa ripoti mapema wiki hii kusema kuwa kenya inawahangaisha wakimbizi wa kisomali ambao imewalazimisha kuchagua kati ya kuondoka nchini humo kwa hiari kwa kukosekana pendekezo mbadala kuhusu cha kuwafanyia wakimbizi hao.

Ripoti hiyo ilisimulia kua serikali ya Kenua imekataa kuwapa wakimbizi hao vyeti vya usajili na kuweza kusihi nchini humo kupata elimu, afya na makaazi hasa kwa sababu wanaonekana kama wahamiaji haramu.

Polisi wa Kenya wamekuwa wakiendesha msako dhidi ya wakimbizi wa kisomali katika harakati zo dhidi ya ugaidi huku wengi wakiwa wamefiksihwa mahakamani.

Makubaliano ya pande tatu, kati ya Kenya, UNHCR na Somalia yaliyotiwa saini mwaka 2013 yaliafikia mpango wa kuwarejesha wasomali Somalia kwa hiari kuanzia mwaka huu 2014.

Shirika la Amnesty limeelezea wasiwasi kuhusu mkataba huu ambao linasema kuwa huenda ukakiuka haki za binadamu