Mugabe ajisikia kama mtoto wa miaka 9

Rais Mugabe ametimiza miaka 90 Haki miliki ya picha Getty

Maelfu ya watu wa Zimbabwe wamehudhuria sherehe rasmi za siku ya kuzaliwa Rais Robert Mugabe.

Bwana Mugabe ambaye ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980, alipeperusha mabofu 90 katika uwanja wa michezo wa Marondera, mashariki ya Harare.

Rais Mugabe, ambaye amerudi punde kutoka Singapore kwa matibabu, alisema ajisikia mzima na kijana kama mtoto wa miaka 9

Aliuambia umati kuwa ushindi aliopata kwenye uchaguzi wa mwaka jana ulishangaza nchi za magharibi zinazomlaumu.

Sherehe hiyo inakisiwa kugharimu dola milioni-moja na hivyo kuzusha malalamiko katika nchi ambayo ina matatizo ya kiuchumi.