Boko Haram: Je Serikali imezembea?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram limekuwa likiwaua watu wasio na hatia Kaskazini mwa Nigeria

Seneta mmoja nchini Nigeria ameelezea gadhabu kuhusu kuzorota kwa usalama na ukosefu wa maafisa wa usalama kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu na kuwaua kufanya shambulizi la pili baya dhidi ya mji mmoja Kaskazini mwa nchi.

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram, waliwaua watu wanne na kuteketeza nyumba zao mjini Izghe siku ya Jumamosi.

Wiki moja kabla ya shambulizi la Jumamosi , zaidi ya watu miamoja waliuawa katika eneo hilo.

Seneta Ali Ndume, alikosoa jeshi kwa kukosa kutuma vikosi katika eneo hilo baada ya shambulizi la kwanza.

Aliongeza kuwa mkakati wa serikali kuhusu usalama na ulinzi umekosa kufaulu.

Serikali ya kitaifa imekosolewa kwa kukosa kuchukua hatua na hata kukosa kuonyesha wasiwasi wowote kuhusu mashambulizi ya Boko Haram dhidi ya watu wasio na hatia.

Boko Haram wamesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka 2009.