Wazuiwa kupinga sheria ya mavazi mafupi

Vazi fupi Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanamama na nguo fupi inayopigwa marufuku Uganda

Polisi wa Uganda wamezuia kundi la wanawake waliopanga kuandamana kupinga sheria inayopiga marufuku picha chafu.

Chini ya sheria hiyo ni marufuku kwa wanawake kuvalia mavazi mafupi, yenye kubana mwilini kiasi cha kuonekana mapaja na makalio na sheti inayoonyesha matiti.

Wanawake hao waliopanga kuandamana mjini Kampala walibeba mabano kupinga sheria mpya baadhi wakuvalia mavazi mafupi. Baadaye walikubaliwa kukusanyika katika uwanja nje ya ukumbi wa kitaifa.