Mpelelezi wa Cuba aachiliwa huru

Mpelelezi mmoja wa taifa la Cuba aliyewachiliwa huru na marekani siku ya alhamisi amepewa makaribisho ya kishujaa baada ya kurejea katika kisiwa hicho cha kikomunisti.

Fernando Gonzalez ni wa pili katika kundi la anachama wa Cuban Five kuachiliwa huru.

Alitumikia kifungo cha zaidi ya miaka 15 jela.

Walipatikana na hatia mnamo mwaka 2001 walipojaribu kuingia katika kambi za jeshi la Marekani mbali na kuwachunguza watu walio mafichoni katika mji wa Miami.

Kesi ya wanachama wa kundi la Cuban Five kwa mda mrefu imeonekana kama kikwazo cha kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.