Gavana akimbiza usalama wake Nigeria

Image caption Gavana wa jimbo la Adamawa Murtala Nyako

Mashambulio ya risasi yamemlazimisha gavana wa jimbo la kazkazini mwa Nigeria la Adamawa kukatisha ziara yake ya kuwatembelea waathiriwa wa ghasia za kiislamu katika eneo hilo.

Gavana huyo Murtala Nyako alikuwa akijaribu kulitembelea eneo ambalo watu 28 waliuawa siku ya Jumatano na washukia wa kundi la Boko Haram.

Alilazimika kuokoa usalama wake baada ya millio ya risasi kukumba kijiji cha kwanza alichozuru.

Wakaazi wa eneo hilo wanadai kwamba wakati wa uvamizi huo wanamgambo wa kundi la Boko Haram walitumia muda mwingi kuwauwa raia kabla ya maafisa wa usalama kuwasili.