Maandamano yashika kasi nchini Venezuela

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji wakipambana na vikosi vya usalama nchini Venezuela

Maelfu ya wapinzani nchini Venezuela wamefanya maandamano katika mitaa mbalimbali mjini Caracas, maandamano yanayofanyika dhidi ya Serikali ya nchi hiyo.

Baada ya maandamano, wanaharakati walipambana na Polisi katika manispaa zinazoshikiliwa na upinzani, Chacao na Altamira.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameahirisha maadhimisho ya sherehe za kitamaduni mpaka mwishoni mwa juma hili na kutoa rai kwa Raia wa Venezuela kusherekea kwa amani.

Takriban watu 17 waliuawa katika vurumai tangu zilipojitokeza zaidi ya majuma matatu yaliyopita.

Viongozi wa upinzani wamewataka watu wapuuzie msimu wa sherehe za kiutamaduni ambazo ni taratibu za jadi ya nchi hiyo kusherekea.

Upinzani unadai kuachwa huru kwa Waandamanaji na Wanaharakati waliokamatwa tangu mwezi uliopita, akiwemo mwanasiasa maarufu Leopoldo Lopez.