Urusi yaimarisha majeshi Crimea

Image caption Jeshi la Urusi Ukraine

Urusi imeendelea kuimarisha majeshi yake ndani ya jimbo la Crimea linalomilikiwa na Ukraine licha ya shinikizo za kidiplomasia kuachana na kitendo chake cha kuingilia nchi huru kijeshi.

Kambi za jeshi la Ukraine zimezingirwa huku rasi hiyo ikitenganishwa kabisa na maeneo mengine, na vizuizi vinaonekana kote barabarani. Mwandishi wa BBC Mark Lowen ametuma taarifa hii.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague ametaja hali nchini Ukraine kama mzozo mkubwa zaidi kuwahi kuikumba Bara Ulaya katika karne ya 21.

Bw. Hague ambaye kwa sasa yuko mjini Kiev ameambia BBC hatua za kidiplomasia dhidi ya Urusi zimeanza kutekelezwa japo kuna taharuki kubwa.

Utawala wa Moscow unasema China inakubaliana na hatua yake ndani ya Ukraine kufuatia mawasiliano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa pande mbili.

Awali nchi kubwa kiuchumi duniani zimelaani Urusi kwa kutuma jeshi lake ndani ya nchi huru.