Hofu ya mauaji ya kimbari CAR

Haki miliki ya picha
Image caption Hali ya wasiwasi imekumba CAR kutokana na vita kutokota

Kuna wasi wasi huenda machafuko ya sasa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati yakageuka na kua mauaji ya kimbari.

Hii ndio maana Umoja wa Mataifa umeahidi kuongeza majeshi la kulinda amani katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.

Kwa sasa maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na wenzao kutoka Bara Ulaya wanshirikiana kushika doria nchini humo.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema wanajeshi wa sasa wataongezwa kufikia 10,000 na polisi 1800.

Bw Moon anataka wanajeshi kupata idhini ya kuhakikisha amani inadumishwa na makundi hasimu pamoja na kupokea ufadhili unaofaa.

Hata hivyo jukumu kuu litakuwa ni kuwalinda raia. Kikosi hiki kitashirikisha jeshi maalum la kukabiliana na wapiganaji wanaolaumiwa kwa mauaji ya raia.

Endapo Umoja wa Mataifa utaidhinisha kutumwa kikosi hiki huenda kikaanza shughuli ifikapo mwezi Septemba.