Uganda kutuma wanajeshi zaidi Somalia

Asakari wa Umoja wa Mataifa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya askari wa Umoja wa mataifa wakiimarisha usalama nchini Somalia

Uganda itatuma kikosi maalum cha askari takriban mia nne katika mji mkuu wa Somali Mogadishu kulinda majengo na ofisi za Umoja wa Mataifa.

Kikosi hicho kinapelekwa mjini humo kufuatia mashambulio dhidi ya ngome za Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Juni na kasri ya rais mwezi uliopita.

Hadi kufikia sasa hali ya usalama imekuwa ikishughulikiwa na kikosi cha Muungano wa Afrika, AMISOM. Tayari Uganda ina askari takriban elfu saba nchini Somalia.

Meya mpya wa mji wa Mogadishu, ambaye alikuwa mwanajeshi pia ameteuliwa.

Waandishi wa habari wanasema uteuzi wa General Hassan Mohamud unaonyesha kuwa kuimarisha hali ya usalama katika mji huo limesalia kuwa muhimu linalopewa kipaumbele na maafisa wa Somalia.