Crimea:kura yapigwa kujiunga na urusi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bunge la Crimea litatoa fursa kwa raia kukubali kujiunga na Urusi au la

Wabunge wa Mji ulio kusini mwa Ukraine,Crimea wamepiga kura ili kuwa sehemu ya Urusi.

Bunge limesema uamuzi huo utaachwa mikononi kwa watu wa Crimea kwa ajili ya kupiga kura ya maoni tarehe 16 mwezi Machi.

Serikali ya Kiev imesema inaamini kuwa Crimea kujiunga na Urusi ni kinyume na Katiba.

Crimea, ambayo wakazi wake walio wengi wana asili ya Urusi, imekua katika malumbano baada ya kuanguka kwa Rais wa taifa la Ukraine.

Taarifa ya Bunge la Crimea imekuja wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujadili hatua ya kupeleka vikosi vya Urusi katika ardhi ya Ukraine.