Jack Wilshere hatoshuka dimbani

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jack Wilshere.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Jack Wilshere atakosa kucheza wiki sita baada ya kupata jeraha la mguu katika mechi aliyochezea England hapo juzi iliposhinda Denmark bao moja kwa bila. Kwa sababu hiyo atakosa mchuano wa FA wa robo fainali hapo kesho dhidi ya Everton na Jumanne ijayo atatazama tu timu yake ikicheza na Bayern Munich katika kombe la kilabu bingwa barani ulaya.

Si hayo tu atakosa mechi nne muhimu za ligii ya England kati ya Chelsea, Manchester City, Swansea na Tottenham ambazo zinacheza mwezi huu.