UN yawaandama FDLR Congo

Mpiganaji wa FDLR Congo Haki miliki ya picha

Askari wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Jamhuri wa Demokrasi ya Congo wameanza operesheni dhidi ya wapiganaji Wahutu kutoka Rwanda wa kundi la FDLR.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani, ambacho kina idhini ya kuwaandama wapiganaji, kinashiriki katika operesheni hiyo Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukitishia kuwa utafanya mashambulio punde dhidi ya FDLR tangu kuwashinda wapiganaji wa M23 wanaoongozwa na Watutsi mwezi Novemba.

Mwandishi wa BBC nchini Congo anasema inaweza kuwa shida kuishinda FDLR kwa sababu wametawanyika katika eneo kubwa na wamechanganyika na wenyeji.