Barcelona kuimarisha soka Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Klabu ya Barcelona ni miongoni mwa vilabu mashuhuri duniani

Klabu ya soka ya Hispania Barcelona, imezindua mpango wa kutoa mafunzo kwa makocha wa Somalia.

Mpango huo ujulikanao kama Futbal Net unalenga kuimarisha soka miongoni mwa vijana nchini Somalia, huku nchi hiyo ikijaribu kujiondoa kutoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kamati ya michezo ya Olimpiki pia inaunga mkono mpango huo.

Wanatumai kufungua vituo kadhaa vya mafunzo kote nchini humo.

Soka na michezo mingine ilikandamizwa na kundi la wanamgambo la Al Shabab kabla ya kuondolewa mjini Mogadishu miaka mitatu iliyopita.