Wanafunzi waandamana Khartoum

Haki miliki ya picha AP

Mwanafunzi mmoja ameuwawa katika maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Maafa hayo yalitokea pale wanafunzi wa Chuo kikuu cha Khartoum walipofanya maandamano.

Kundi la kutetea haki za binadamu Amnesty International, limesema mwanafunzi huo alifariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya makundi ya kiusalama kuwatawanya wanafunzi hao kwa kuwashambulia kwa risasi, na vitoa machozi.

Ni ghasia za kupinga machafuko yanayozidi huko Darfur.

Machafuko zaidi yatarajiwa

Zaidi ya watu milioni mbili wamehamishwa makwao tangu waasi walipoanza kukabiliana na serikali mwaka 2003.

Machafuko huko Darfur sasa yameingia katika jiji kuu Khartoum, pale mwanafunzi wa chuo kikuu alipouwawa.

Machafuko hayo ya Jumanne yanania ya kuleta amani magharibi mwa Sudan, na ni mabaya zaidi kuwahi kutokea mjini Khartoum tangu Septemba mwaka jana ambapo maelfu ya watu walifanya maandamano katika barabara za mji huo baada ya serikali kukataa kupunguza bei ya mafuta.

Katika taarifa kwenye mtandao wa Wizara ya ndani ya taifa hilo, polisi hawajasema ni nini kilichomuuwa mwanafunzi huyo wa chuo kikuu cha Khartoum.