Huwezi kusikiliza tena

Nani wezi wa talanta Afrika?

Wengi wa wanamuziki mashuhuri wa nchi zinazozungumza Kifaransa barani Afrika - Alpha Blondy, Tiken Jah Fakoly na Magic System - ni wazaliwa wa Ivory Coast.

Lakini kwa sababu ya wizi wa kazi za sanaa, wasanii hawanufaiki kama inavyostahili.

Inakadiriwa asilimia 80 ya mapato yao huishia kwenye CD za wizi na watu kuzirekodi bila ruhusa ya wamiliki.

Lakini katika mradi wa aina yake Afrika Magharibi, serikali ya Ivory Coast imeivalia njuga biashara hii haramu. Joan Simba anatuarifu zaidi.