Kesi dhidi ya Vigogo wa Sudan:K yaendelea

Image caption Pagan Amum

Kesi dhidi ya viongozi wanne wa kisiasa nchini Sudan Kusini ambao wanakabiliwa na mashitaka ya uhaini imeingia siku yake ya pili hii.

Upande wa mashitaka umewataka viongozi saba walioachiliwa kwa dhamana Januari, ambao kwa sasa wako nchini Kenya pia wafunguliwa mashitaka.

Viongozi hao wanadaiwa kuwa walijaribu kuipindua serikali ya rais Salva Kiir Disemba mwaka uliopita.

Wote mhao walifikishwa mbele ya mahakama leo ingawa wamekanusha madai haya.

Pagan Amum, aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha SPLM, aliyekuwa waziri wa ulinzi Majak d'Agoot, aliyekuwa waziri wa usalama wa katika ofisi ya Rais na balozi Ezekiel Gatkuoth Lol,

Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo dhidi ya viongozi hao wanne wa kisiasa wa Sudan Kusini aliieleza mahakama kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka viongozi wengine saba walioachiliwa kwa dhamana na sasa wako katika nchi jirani ya Kenya.

Aliiambia mahakama kuwa ushahidi walio nao unaonyesha kuwa wanasiasa hao walishirika katika msururu wa mikutano ya kupanga njama ya kuipundua serikali ya Salva Kiir Mayardit.

Viongozi hao saba waliachiliwa kwa dhamana mwisho wa Januari, baada ya shinikizo kali kutoko kwa jamii ya kimataifa na kukabidhiwa rais Kenyatta wa Kenya.

Mwendesha mashtaka anataka wafikishwe mahakamani wiki ijayo wakati kesi hiyo itasikizwa tena.

Hata hivyo, haitakuwa kazi rahisi, kwa sababu kwa sasa wanashiriki katika mazungumzo ya amani yanayo enedelea mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kesi hii imezidi kuvutia hisia kali nchini humo. Makahama leo ilijaa pomoni na raia ambao wengi walionekana kuunga mkono washukiwa hao wanne ambao wamekanusha madai yote 11, ikiwemo shtaka la uhaini dhidi yao.

Hata hivyo kuna baadhi ambao wanataka kesi iendelee ili haki itendeka iwapo walihusika na machafuko hayo.

Lakini kuna wasiwasi iwapo kesi hii itaendeshwa kwa njia ya haki, na kumaliza vita nchini humo, kutokana na kuwa, mahakama ya juba inasimamiwa na rais Salva Kiir ambaye amesema walipanga kuipindua serikali yake.