Mashambulizi mapya dhidi ya Al-Shabaab

Haki miliki ya picha AFP ONU UA
Image caption Wanajeshi wa AU Somalia

Wanajeshi wa Muungano wa Afrika wakishirikiana na wanajeshi wa Somalia, wameanza mashambulizi mapya dhidi ya kundi la wanamgambo la Al Shabaab.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa wamezindua oparesheni ya kushambulia ngome mbili zinazotumiwa na wanamgambo hao katika eneo la Hiraan.

Wanajeshi wa Ethiopia wanaelekea katika ngome kuu ya wanamgambo hao ya Buloburde, wakati kikosi cha wanajeshi kutoka Djibouti kikielekea katika ngome ya Bukakable.

Watu wengi wanaripotiwa kutoroka maeneo hayo. Miji mitano ilikombolewa wiki jana kutoka kwa Al shabaab Magharibi mwa Somalia.

Al Shabaab walitumiliwa kutoka mji mkuu Mogadishi katika mashambulizi makali yaliyofanywa na AU pamoja na wanjeshi wa Kenya na Somalia.

Hata hivyo wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kuvizia huku wakilenga hata ikulu ya Rais mjini humo.