Wanajeshi washambuliwa Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Misri wakiwa ndani ya Kifaru

Televisheni ya taifa ya Misri imetangaza kuwa mwanajeshi mmoja amepigwa risasi na kuawa watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na kufunika nyuso zao

Watu hao wasiojulikana walishambulia basi la kuwabeba wanajeshi.

Maafisa kadha walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo la kwanza kuwahi kutokea katika mji mkuu Cairo.

Shambulizi hili limefanyika siku moja kabla amiri mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi atangaze wazi niya yake ya kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Al sisi ndiye aliyeongoza mapinduzi yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi na kundi lake la Muslim Brotherhood