Marekani na vifaa vipya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisa wa kijeshi wa Marekani

Maafisa wa Marekani wanaosaidia kaisaka ndege ya Malyasia iliyotoweka Jumamosi iliyopita, wanasema kuwa taarifa mpya sasa inawaelekeza hadi Magharibi mwa bahari ya Hindi.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa huenda ndege hiyo ilikuwa ikituma data katika mtambo wa setllite kwa muda wa masaa manne baada ya kutoweka kutoka katika mitambo ya rada ikiwa njiani kuelekea Beijing.

Wanajeshi wa majini wa Marekani imetuma meli iliyo na Helikopta kadhaa hadi katika eneo mpya ndani ya bahari ya Hindi.

Maafisa wa serikali ya Marekani wameiambia shirika la habari la ABC kuwa vitengo viwili vya mawasiliano katika ndege iliyopotea ilikwama kuwasilisha data kwa muda tofauti, kumaanisha kuwa janga baya halikutokea.