Nani aliiba saa za Pistorius?

Image caption Oscar Pistorius mahakamani

Saa mbili za kifahari za Oscar Piatorius zilitoweka katika eneo la tukio la mauaji ya mpenzi wake, polisi mstaafu aliifahamisha mahakama inayosikiliza kesi ya mauaji dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu.

Polisi huyo kwa jina Schoombie van Rensburg, aliambia mahakama kuwa alikasirishwa sana na kupotea kwa saa hizo na kwamba aliamuru polisi kukaguliwa.

Mahakama pia ilionyeshwa picha ya Pistorius ikiwa amevalia nguo iliyokuwa na damu.

Amekana madai ya kumuua mchumba wake Reeva Steenkamp mwaka jana akisema kuwa alifyatua risasi akidhani jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka umesema kuwa Pistorius alimuua mchumba wake kwa maksudi baada ya wawili hao kuwa na ugomvi wa kinyumbani mwaka jana.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Jumatatu.