Malaysia yaomba data kutoka nchi kadhaa

Marubani wa ndege iliyopotea

Wizara ya usafiri ya Malaysia inasema kuwa imeomba ushirikiano wa nchi zote kwenye njia mbili ambapo ndege iliyopotea juma lilopita huenda kuwa imepita.

Imeomba msaada wa data kutoka Satelite na Radar na msaada katika shughuli za msako.

Uchunguzi piya unafanywa kuhusu marubani wawili wa ndege hiyo na nyumba zao zimepekuliwa.

Polisi wa Malaysian wanasema piya wanachunguza historia ya wafanyakazi wengine wa ndege na abiria wote pamoja na wahandisi waliohudumia ndege hiyo.

Waziri wa Usafiri, Hishammuddin Hussein, alisema sasa nchi 25 zimehusika katika msako.

Alisema sasa wanalenga zaidi njia mbili ambazo pengine ndege hiyo ilifuata - kaskazini au kusini.