Zogo Sudan wananchi wakidai haki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wananchi wanaandamana kudai wanachosema ni haki zao

Polisi katika mji mkuu wa Sudan -Khartoum Jumamosi walitumia gesi ya kutoa machozi kuvunja maandamano ya zaidi ya watu 200 waliokuwa wanapinga serikali ya Rais Omar al Bashir.

Walioshuhudia wanasema kuwa Polisi walilazimika kutumia gesi hiyo kuwaondoa waandamanaji hao kutoka katika barabara za mji mkuu.

Baadhi ya waandamanaji walifoka huku wakitaka uhuru na haki kufanyika kote Nchini humo na hata kushambulia maafisa wa polisi kwa mawe.

Hiyo ni maandamano ya pili ya aina hiyo kufanyika juma hili. Mwanafunzi mmoja aliuwawa katika maadamano ya awali siku ya jumanne iliyopita wakati wa ghasi