Mazoezi makali yanazuia Mafua

Image caption Kufanya mazoezi kunaweza kukusaidia kuodnokana na mafua

Kufanya mazoezi makali katika kipindi cha saa mbili unusu kila wiki inaweza kukuzuia kupatwa na mafua.

Hivi ndivyo utafiti uliofanywa na chuo cha mafunzo ya afya na magonjwa ya Tropiki mjini London, Uingereza (London School of Hygene), ulivyogundua.

Takriban watu 4,800 walishiriki katika utafiti huo uliofanywa kwa njia ya mtandao kwa kuhoji watu na kurekodi majibu yao.

Mwanzo walitakiwa kurekedi, umri wao, ikiwa wana watoto na ikiwa wamepata chanjo ya Mafua.

Mazoezi ya kiwango cha kadri hayakuwa na uwezo wowote wa kukuzuia mafua.

Image caption Kwa mujibu wa utafiti huu, mazoezi makali ni kama kuendesha baiskeli na kukimbia

Utafiti huu ambao umeendelea kwa miaka mitano sasa unajaribu kuona wanaopata na wasiopata mafua.

Moja ya swali ambalo waliloulizwa ni mara ngapi wao hufanya mazoezi makali kwa wiki, kama kukimbia , kuendesha baiskeli na kushiriki mashindano angalau kwa saa moja hadi tano kwa wiki.

Watu hao walitakiwa kushiriki utafiti huo kila wiki , kurekodi wanavyohisi na ikiwa wana dalili zozote za mafua.

Waliokwepa mafua.

Watafiti walisema kuwa matokeo ya utafit wao yanaonyesha kuwa kati ya watu elfu moja, 100 wanaweza kujizuia na mafua ikiwa watafanya mazoezi makali kila wiki.

Hata hivyo mmoja wa watafiti Daktari, Alma Adler, amesema kuwa matokeo hayo sio kamilifu, yanahitaji uchunguzi zaidi ingawa yanaonyesha manufaa ya kufanya mazoezi ili kulinda mwili.