Ukabila wasababisha mauaji Nigeria

Image caption Jamii ya Fulani ni ya wafugaji wa kuhamahama

Watu 100 wakazi wa kijiji kimoja wameuawa katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria, katika shambulizi ambalo limehusishwa na uhasama kati ya jamii mbili.

Watu waliokuwa wamejihami vikali, walivamia vijiji vitatu, katika wilaya ya Kaura Kusini mwa jimbo hilo na kusababisha maafa hayo.

Haijulikani hasa nani aaliyepanga mashambulizi hayo, lakini wakazi wanalaumu watu kutoka jamii ya wafugaji ya Fulani.

Maeneo ya kati mwa Nigeria, yamekuwa yakishuhudia ghasia za mara kwa mara ambazo zinasemekana kutokana na mizozo ya ardhi na dini.

Maelfu ya watu hata hivyo wameuawa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni kwenye vita kati ya jamii ya wahamiaji ya Fulani na wenyeji wakulima.

Mbunge kutoka jimbo hilo Yakubu Bitiyong, alizuru, eeo la mauaji amabyo inaarifiwa yalifanyika siku ya Ijumaa.

Wengi wa waliouawa katika vijiji vya Ugwar Sankwai, Ungwan Gata na Chenshyi, waliteketea sana kiasi cha kutoweza kutambuliwa.

Bwana Bitiyong alisema kuwa washambuliaji wawili waliuawa.

Mashambulzi haya ya Kaduna yametokea, siku moja tu baada ya taarifa za mauaji ya watu 69 katika jimbo la Katsina.