Chelsea yamenyana na Galatasaray

Image caption Drogba, Eto'o na Lampard ni miongoni tu mwa wanaoshiriki mechi hii

Mchezaji wa Cameroon Samuel Eto'o yuko katika msitari wa mbele leo katika mechi kubwa dhidi ya Galatasaray katika mkondo wa pili wa michuano ya klabu bingwa ulaya katika uwanja wa Stamford Bridge.

Eto'o alikuwa amepumzishwa katika mechi ya Premier League ambayo Chelsea ilishindwa na Aston Villa mwishoni mwa wiki.Tayari ameingiza bao la kwanza.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anamchezesha Eto'o badala ya Fernando Torres, ambaye sasa ni mchezaji wa akiba licha ya kuingiza dhidi ya Glatarasaray katika mechi yao ya kwanza mjini Istanbul.

Frank Lampard naye amechukua nafasi ya Nemanja Matic.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba yuko miongoni mwa wachezaji wa kwanza kuingia uwanjani kuwakilisha Galatasaray huku ikiwa ni mara yake ya kwanza kurejea Stamford Bridge tangu mwaka 2012.

Nani unadhani ataibuka mshindi leo?