Dortmund 5 - 4 St Petersburg

Image caption Borussia Dortmund vs Zenit st Petersburg

Borussia Dortmund ilifuzu kwa hatua ya robo fainali licha ya kuambulia kichapo cha 1-2 mikononi mwa Zenit St Petersburg huko Ujerumani .

Dortmund iliyoshindwa na Bayern Munich katika fainali za kombe la mabingwa Uropa mwaka uliopita ilikuwa imejiweka kifua mbele baada ya kushinda mechi ya mkondo wa kwanza kwa mabao 4-2

itakuwa kwenye droo ya robo fainali siku ya ijumaa baada ya kusajili ushindi wa jumla ya mabao 5-4.

Zenit, ilikuja Ujerumani ikiwa tayari imemfuta kazi Luciano Spalletti sasa itakuwa chini ya Kocha Andre Villas-Boas kuanzia leo .

Mchezaji kutoka Brazil ,Hulk ndiye aliyewaweka wageni hao mbele kunako dakika ya 16 lakini Sebastian Kehl akaisawazishia Dortmund kunako dakika ya 38.

Licha ya bao la Jose Rondon 73 st Petersburg haikuweza kusonga mbele.

Dortmund hata hivyo itakuwa na kibarua kigumu katika mkondo wake wa kwanza kwani Marco Reus na nyota wao Robert Lewandowski kuadhibiwa kwa kucheza visivyo .

Lewandowski hatoruhusiwa kushiriki mkondo wa kwanza wa robo fainali.

Dortmund sasa inajiunga na Bayern Munich, Paris Saint Germain, Real Madrid ,Athletico Madrid, Barcelona, Manchester United na Chelsea katika hatua ijayo ya robo fainali.

Droo ya robo fainali itafanyika Ijumaa .