Je Manchester United watajikwamua?

Image caption Moyes ana matarajio makubwa

Meneja wa Manchester United David Moyes anajitahidi kuhakikisha mabadiliko yananadhihirika leo wakati klabu yake itakapomenyana na Olympiakos katika mchuano muhumi wa ligi ya klabu bingwa Ulaya

Kwa hilo, amemleta mchezaji wa kiungo cha kati Ryan Giggs kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoanza mechi yao muhimu nyumbani Old Traford.

United watasaka mabao leo kwa udi na uvumba dhidi ya timu ambayo ina wachezaji mahiri pia. Moyes ameweka Antonio Valencia kushirikiana na Danny Welbeck huku Wayne Rooney akishirikiana na Robin van Persie mbele.

Yote tisa, kumi ni kwamba Moyes alifanya mabadiliko manne siku ambayo walipigwa mabao 3 kwa nunge na Liverpool.

Giggs, mwenye umri wa miaka 40,ni mmoja wa wachezaji wenye uzoefu zaidi katika mechi za klabu bingwa ulaya ingawa amecheza mara mbili tu tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Olympiakos ambao ni mabingwa wa Ugiriki, ilifanya mabadiliko machache sana ya mchezaji mmoja tu katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Nani unadhani ataondoka uwanjani na pakacha la mabao? Andika ujumbe wako kwenye ukurasa wetu wa Facebook https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209?ref=hl