Kauli yako:Vipi ndege imetoweka isijulikane iliko?

Haki miliki ya picha 1
Image caption Jamaa za abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wametishia kususia chakula

Uchunguzi kuhusiana na ndege ya Malaysia iliyotoweka ikiwa na abiria mia mbili thelathini na tisa unaendelea, huku kukiwa na habari za kutatanisha kuihusu.

Hakuna kilichopatikana na kusemekana kuhusishwa na ndege hiyo yenye nambari ya usajili MH370 iliyotoweka siku kumi na mbili zilizopita, ikiwa njiani kutoka Kualar Lumpur kuelekea Beijing.

Katika mjadala wetu wa leo kwenye Dira ya Dunia tunatathmini tukio hilo na tunauliza ni vipi ndege kubwa kama hiyo, itoweke kabisa licha ya kuwepo kwa utaalamu na vifaa vya kisasa?

Jiunge na Robert Kiptoo akiwahoji wataalamu kuhusu tukio hili. Kupitia mtandao wetu http://www.bbc.co.uk/swahili/

Changia mjadala wetu kwenye ukurasa wetu wa Facebook https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209.