Hali ya taharuki yatanda Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption taharuki yatanda Ukraine baada ya afisa wa jeshi kupigwa risasi

Hali ya wasiwasi imetanda eneo la Crimea kufuatia kuuawa kwa afisa mmoja wa kijeshi kwa kupigwa risasi.

Jeshi la Ukraine lilisema kuwa afisa huyo aliuawa wakati watu wenye silaha waliokuwa katika sare za kijeshi za Urusi walipofyatulia risasi kituo kimoja cha kijeshi cha Ukriane cha Kiev.

Afisa huyo ameuawa saa chache baada ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov kumuonya mwenzake wa Marekani, John Kerry kuwa vitisho vya Marekani vya kuwekea taifa lake vikwazo vya aina yo yote baada ya

Crimea kutangazwa na Urusi kuwa sehemu moja ya taifa hilo si haki. Urusi imesema inatafakari hatua zitakazochukuliwa na mataifa ya Magharibi kabla ya kuamua la kufanya.

Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Obama na Chansela wa Ujerumani Angela Markel wamekubaliana katika mashauriano kwa njia ya simu kuwa wachunguzi wa kimataifa wanapaswa kutumwa Kusini na Mashariki mwa Ukriane

kufuatia uamuzi wa Urusi kuchukua sehemu ya Crimea kutoka kwa Ukraine.

Maafisa hao wa Ikulu walisema viongozi hao wawili walishutumu hatua ya Rais wa Urusi Putin ya kutangaza eneo hilo kuwa chini ya Urusi baada ya kura ya maoni.

Hata hivyo walisema kuwa njia za kidiplomasia zingali wazi kuhusiana na hali hiyo.

Mnamo Jumatano Makau wa Rais wa Marekani alisema huo ulikuwa unyakuzi wa ardhi.

Juma lililopita Marekani na Jumuiya ya Ulaya walisema watapiga tanji mali ya viongozi fulani wa Urusi na Ukraine na pia kuweka masharti magumu ya wakaazi wa Urusi kutembelea mataifa hayo ya Magharibi.