Hoja:Nini kinavunja ndoa nyingi siku hizi?

Image caption Masiah ya ndoa siku hizi yanasemekana kuwa na changamoto nyingi sana

Kuvunjika kwa ndoa ni jambo ambalo katika jamii nyingi za kiafrika lilikuwa gumu kutokana na misingi ya tamaduni na mila ambazo zilikuwa na mbinu za utatuzi wa migogoro na kuhakikisha wanandoa hawaachani.

Lakini kadri ya miaka inavyozidi kwenda mbele inaonekana ni rahisi wanandoa kufikia hatua ya kutamkiana wazi kuwa sasa basi na kweli inakuwa basi.

Wazee walioishi chini ya mila na desturi za zamani wanakosoa mfumo wa ndoa uliopo sasa na kudai kuwa mifumo yao ya kale ilikuwa mizuri. Kwa nini Ndoa zinavunjika kwa urahisi siku hizi?Je mifumo ndio mibaya au?

Huwezi kusikiliza tena

Jiunge na mjadala huu kwenye ukurasa wetu wa Fecebook

Mwandishi wa BBC Dar es Salaam Leonard Mubali pia anaangazia hali ya ndoa nchini Tanzania kwa kuzungumza na machifu wa jadi akianza na chifu Mleshelwa Mwene Nzunda kutoka wilayani Mbozi mkoani Mbeya pamoja na baadhi ya wanandoa na watarajiwa wa sasa.