Mwanawe rais 'alipora' mali ya umma?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Teodorin Obiang anadaiwa kupora mali ya umma na kujinunulia majumba na magari ya kifahari Ufaransa

Uchunguzi umeanzishwa rasmi dhidi ya mwanawe Rais wa Equatorial Guinea,Teodorin Obiang nchini Ufaransa.

Obiang anatuhumiwa kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia haramu.

Mahakimu nchini Ufaransa wamekuwa wakiendesha uchunguzi dhidi ya viongozi wa nchi hiyo tangu mwaka 2010.

Wengi wanadaiwa kuhusika na uporaji wa pesa za umma huku wakijinunulia mali nyingi katika nchi za kigeni hususan nchini Ufaransa.

Bwana Teodorin Obiang amekana kuhusika na wizi akisema kuwa mali yake ambayo imemuwezesha kununua nyumba ya kifahari mjini Paris ,ndege ya kibinafsi na magari ya kifahari ameipata kwa njia halali.

Pia anakabiliwa na tuhuma za wizi wa pesa nchini Marekani.