Huwezi kusikiliza tena

Chupa ndogo hatari kwa walevi DRC

Unywaji wa pombe umeongezeka kwa kiasi kikubwa mjini Kinshasa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na utengenezaji wa chupa ndogo za pombe ambazo ni za bei nafuu.

Kwa kawaida aina nyingi za bia nchini humo zimekuwa zikipakiwa katika chupa za lita moja kiasi ambacho walevi wengi hawawezi kumudu.

Lakini sasa chupa ndogo zilizotengezwa zimevutia watu wengi wasiojiweza kiuchumi na sasa vijana pia wameanza ulevi.