Malaysia:Shughuli zaendelea kuisaka ndege

Haki miliki ya picha AMSA
Image caption Picha za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia nchini Australia

Ndege na meli kutoka nchi mbali mbali zinaendelea kuitafuta mabaki ambayo huenda yanatokana na ndege ya Malaysia iliyopotea takriban wiki mbili zilizopita ikiwa imebeba takriban watu 240.

Matumaini ya kutatua kitendawili hicho yaliongezeka baada ya Australia kutoa picha za Satelaiti za vitu viwili vilivyoonekana baharini vuikidhaniwa kuwa vifusi vya ndege hiyo.

Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna cha maana kilichopatikana.

Afisa mmoja mkuu wa New Zealand amesema operesheni hiyo ilitatizwa na kuchafuka kwa bahari na kutoona vizuri.

Meli ya mizigo ya Norway ilitumia taa kuyatafuta mabaki hayo pasina kufanikiwa.