Mtandao wa twitter kufungwa Uturuki

Twitter Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtandao wa kijamii wa Twitter wafungwa Uturuki

Mtandao wa kijamii wa , Twitter, unafungwa nchini Uturuki , saa chache baada ya waziri mkuu , Recep Tayyip Erdogan, kuahidi kuuondoa .

Bwana Erdogan -- ambaye anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa uchaguzi kuwa hajali kuhusu namna jamii ya kimataifa itakavyochukulia hatua yake .

Neelie Kroes, ambaye ni naibu rais wa tume ya muungano wa Ulaya amesema umamuzi wa kufungwa kwa mtandao huo ni wa kulaumiwa .

Serikali ya Bwana Erdogan imekuwa ikilalamika kuwa mtandao wa Twitter ulipuuza uamuzi wa mahakama ulioitaka viunganishi vya taarifa zake vinashukiwa kurekodi mawasiliano yake binafsi.