Yachukua miaka 60 kujenga hospitali DRC

Rais Kabila wa DRC Haki miliki ya picha AFP

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo amefungua hospitali mjini Kinshasa miaka 60 tangu hospitali hiyo kuanza kujengwa.

Waziri wa Afya, Felix Kabange Numbi, alisema hiyo ndio hospitali yenye vifaa vya kisasa kabisa nchini humo.

Ilianza kujengwa mwaka wa 1954 lakini ujenzi ukasimama wakati wa uhuru mwaka wa 1960 na kuanza tena miaka mingi baadae.

Hospitali hiyo hatimae ilimalizwa na Uchina miaka mitatu iliyopita lakini haikuweza kufunguliwa kwa sababu ya uhaba wa vifaa na wafanyakazi wenye ujuzi.