Refa ajutia kadi nyekundu kwa Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Refa wa mchezo kati ya Chelsea na Arsenal akitoa kadi kimakosa

Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya kufanya makosa kwenye michuano ya ligi kuu kumwondoa kimakosa mchezaji wa Arsenal wakati timu hiyo ilipopoteza mchezo kwa kuchapwa magoli 6-0 na Chelsea.

Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini Kieran Gibbs aliondolewa kimakosa

Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.

Hata hivyo baadae Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika mchezo huo.

Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi