Barcelona yaipa kichapo Real Madrid

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi

Kocha wa Barcelona Gerardo Martino amesema La Liga ndo imeanza baada ya timu yake kuleta matumaini ya kutwaa ubingwa kwa kuifunga Real Madrid mabao 4-3.

Lionel Messi aliifungia timu yake mabao matatu, hivyo Barcelona imepanda kwa utofauti wa alama moja na wanaoongoza ligi hiyo, Atletico Madrid na Real Madrid iliyo nafasi ya pili.

Kocha Gerardo ametamba kuwa wamerudi kupigania ushindi kwenye Ligi hiyo na kuwa alikuwa na uhakika kuwa timu hizo tatu zitakuwa zikipambana kuwania ubingwa.

Messi anachukua nafasi ya pili, kuwa mfungaji bora katika Ligi ya La Liga akiwa na magoli 236.